.Na Caleb Otieno

Ugonjwa wa Covid-19 umesababisha mataifa mengi Barani Afrika kufunga maeneo mengi yakiwemo ya biashara na burudani ili kudhibiti kuenea kwa Virusi vya Corona. Hii imeleta ongezeko la matumizi ya Intaneti-iwe ni masomo kupitia mtandao, kutekeleza majukumu ya kikazi kutoka Nyumbani, shuguli za mawasiliano na hata sekta ya afya. Changamoto: Wakati mwingine unapata kwamba kampuni moja ya mawasiliano iko na Intaneti yenye kasi  nzuri, lakini bei iko juu sana. Pia unapata kampuni nyingine ina Intaneti ya bei nafuu,” lakini sio ya kutegemewa unaponunua”. Japokuwa matumizi ya Intaneti yameongezaka Wakati huu wa maambukizi ya Corona, zaidi ya asilimia 60% ya watu Barani Afrika bado hawajafikiwa na teknolojia ya 4G, kwa mujibu wa takwimu za Benki ya Dunia.

A client at Ashen Books Cyber Cafe in Kitengela

Changamoto Hizi Zinaweza Tatuliwa Vipi Ili Afrika Isibakie Nyuma Katika Mabadiliko Ya Kiteknolojia Yanayoendelea? Rais wa shirika la Internet Society Kenya (ISOC Kenya) Wainaina Mungai anasema.

Makampuni nyingi ya huduma za mitandao zinakabiliwa na Gharama kubwa ya kuwekeza Katika miundombinu hitajika Kama vile mabomba na nyaya kutoka mijini hadi mikoani na vijijini. Pia serikali zinafaa kuzingatia kuweka huduma za Intaneti Kama vile Wi-Fi Katika maeneo Fulani ili wananchi waweze kupata huduma hizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *